HUU NDIO UTAJIRI WA KWANZA
Watu wengi sana katika maisha ya leo wako mbio wakitafuta pesa bila kuangalia wanapita wapi au wanafanya nini, lengo lao la msingi likiwa ni lazima pesa ipatikane. Bahati mbaya sana katika mbio hizi mara nyingi afya husahaulika sana, kwa kuonekana kwake labda sio muhimu sababu mtu anajiona yuko fit tu anachelewa kulala, anawahi kuamka, hapati muda wa kupumzika, na mambo mengine mengi sana. Lakini siku moja itafika ukawa na pesa zote ulizohitaji (kama utazipata) lakini huenda afya yako ikawa mbovu na ukaanza mbio nyingine tena za kukimbilia kuiokoa afya ambayo sasa itakunyima hata uhuru wa kufurahia pesa zako. Kwahiyo wito wangu ni kwamba kamwe tusisahau afya kwa haswa ndio utajiri wa kwanza.